March 26, 2018



Na George Mganga
 
Kuelekea mchezo wa kirafiki wa kimataifa Jumanne ya kesho, Kocha wa DR Congo, Florent Ibenge, amesema mechi hiyo itakuwa ngumu.

Ibenge ameeleza mechi hiyo haitakuwa rahisi kutokana na Taifa Stars kupoteza mechi iliyopita dhidi ya Algeria kwa jumla ya mabao 4-1 huko Algiers.

Kocha huyo anaamini haitouwa rahisi kwa Tanzania kukubali kupoteza tena kesho hivyo watapambana kupata matokeo.

"Utakuwa mchezo mgumu kwa sababu Taifa Stars ilipoteza mchezo wake uliopita, hivyo hawatotaka kupoteza tena mchezo mwingine" amesema Ibenge.

Aidha, Ibenge amesema wameamua kuja kucheza Tanzania kwasababu Stars ni timu nzuri na vilevile ni majirani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic