March 26, 2018



Na George Mganga

Kocha Msaidizi wa Taifa Stars, Hemed Morocco, amesema maandalizi ya mchezo wa kesho dhidi ya Congo yameenda vizuri lakini mechi haitakuwa mrahisi.

Morocco ameyasema hayo ikiwa imesalia siku moja ambayo ni leo kuelekea mchezo huo wa kirafiki wa kalenda ya FIFA utakaopigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kuelekea mchezo huo, Morocco amesema Stars itawakosa wachezaji, Abdulazizi Makame ambaye aliumia mazoezini pamoja na Mlinda Mlango Aishi Manula ambaye bado hajapona majeraha yake.

Kukosekana kwa Manula kutamfanya Golikipa aliyeanza dhidi ya Algeria, Mohammed Abdulrahman kuanza dhidi ya Congo pia.

"Tutawakosa Aishi Manula ambaye bado hajawa fiti, hivyo kipa aliyeanza dhidi ya Algeria ataendelea kuwa langoni, vilevile Makame naye hatoweza kucheza baada ya kuumia mazoezini" amesema Morocco.

Mbali na hayo, Morocco amesema wanahitaji kushinda mechi hiyo ili wajiweke pazuri katika viwango vya ubora wa soka duniani (FIFA).

1 COMMENTS:

  1. Kipa gani uyoooo hata cross wanatoka wakati hana uhakika daaah...si angedaka hata kabwir

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic