MASAU: TUNAPAPASA KILA ANAYEKUTANA NASI KWA SASA, NJOMBE MJI WAJIANDAE LEO
Na George Mganga
Kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara mchana wa leo, Afisa Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema timu yake itaendeleza kutumia mfumo wake mpya wa kupapasa.
Ruvu Shooting itakuwa mgeni kucheza dhidi ya Njombe Mji, mechi itakayopigwa kwenye Dimba la Sabasaba mjini Njombe.
Masau amesisitiza hivi sasa watakuwa wanapapasa tu kila timu wanayokutana nayo kwa maana kikosi chao kiko vizuri, huku akiwaasa mashabiki wa Ruvu wajitokeze kwa wingi Uwanjani kupata alama 3 muhimu.
"Tumekuja Njombe kuendeleza mfumo wetu wa kupapasa, hatuoni namna ya kupoteza mchezo huu hata kama tupo ugenini, nawaomba mashabiki watupe sapoti ya kutosha, kwani hatutawaangusha kupata alama 3 leo" amesema Bwire.
Mechi hii itaanza majira ya saa 8 mchana wa leo na itakuwa mbashara kupitia king'amuzi cha Azam TV.
0 COMMENTS:
Post a Comment