POGBA HATAKI KUMZUNGUZIA JOSE MOURINHO, TETESI ZINGINE KUHUSU SOKA LA ULAYA HIZI HAPA
Juventus wako katika mipango ya kumsajili beki kutoka Arsenal, Hector Bellerin (22) ambaye milango yake ya kuondoka ipo wanzi ndani ya timu hiyo. Guardian
Kocha Jose Mourinho, amesema hadhani kama kiungo wake Mbelgiji, Marouane Fellain ataendelea kusalia ndani ya kikosi chake mara baada ya mktaba wake kumalizika. Mail.
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola, amepanga kufanya usajili wa wachezaji wawili au mmoja pekee katika msimu wa majira ya joto ili kukipa nguvu kikosi chake. Telegraph.
Kiungo Mfaransa (24), Paul Pogba, amesema hataki kuzungumzia suala la mahusiano yake na Kocha Jose Mourinho namna yanavyoendelea hivi sasa, ikumbukwe wawili hawa wameripotiwa kutokuwa na maelewano. Express.
Baadhi ya vilabu kutoka Uingereza, vinatamani kumsajili mshambuliaji Mario Balotelli anayekipiga Nice ya Ufaransa.
0 COMMENTS:
Post a Comment