March 26, 2018





 Bondia wa ngumi za Kulipwa nchini, Bruno Tarimo 'Vifuaviwili' amewasili nchini leo mchana akitokea Australia baada ya  kufanikiwa  kushinda mkanda wa ubingwa wa WBA Oceania kumtwanga kwa pointi mpinzani wake, Billel Dib 'Baby Face' raia wa Australia.

 Pambano hilo la raundi kumi ambalo lilifanyika  wikiendi iliopita  kwenye Ukumbi wa Seagulls Rugby League Club, uliopo katika Mji wa  Tweed Heads kwenye Mkoa wa  New South Wales, Australia.
Bruno nakuwa ni bondia wa pili kutoka katika Gym ya Sharif, Bagamoyo Pwani kufanikiwa kushinda ubingwa nje ya ardhi ya Tanzania baada ya hivi karibuni, bondia Maoni Ally kushinda ubingwa wa WBC nchini Afrika Kusini.

Mara baada ya kutua nchini, Vifuaviwili alisema kuwa ushindi wake umetokana na kufanya mazoezi kwa juhudi kabla  pambano hilo huku akisisitiza hakutaka kuwaangusha Watanzania ndiyo maana amefanya kweli.

"Nashukuru nimerejea nyumbani na ubingwa ambao Watanzania walinituma huko nilipotoka kwa sababu sikutaka kuwaangusha licha mpinzani wangu kuwa bora ndani ya ulingo kwa kuwa alinisumbua lakini sikutaka kuwaangusha mlionitunma ubingwa huu," alisema  Bruno Vifua Viwili.


1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic