March 26, 2018




Beki wa kati wa Kagera Sugar, Juma Nyosso, amefunguka kuwa, kwa sasa amebakiza mechi moja tu kati ya zile tano alizotakiwa kuzikosa baada ya kusimamishwa na Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Soka Tan­zania (TFF), hivyo ana­jiandaa kurudi kuiokoa timu yake hiyo.
 
Nyosso ambaye aliwahi kuichezea Simba, alisimamish­wa kucheza mechi tano za Ligi Kuu Bara baada ya kukutwa na kosa la kumshambulia shabiki wakati timu yake ya Kagera Sugar ilipokubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Simba, Janu­ari 22, mwaka huu.

Mechi alizokosa Nyos­so kutokana na adhabu hiyo na matokeo yalivy­okuwa ni hizi; Kagera 1-1 Singida United, Kagera 2-1 Majimaji, Yanga 3-0 Kagera na Kagera 1-0 Mwadui. Mechi ijayo dhidi ya Ndanda, ndiyo ya mwisho.
Kagera Sugar ambayo kwa sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 21, imebakiwa na mechi nane ambazo inatakiwa kuzitumia vizuri ili isishuke daraja mwishoni mwa msimu huu.
  
Nyosso amesema: “Mechi ijayo dhidi ya Ndanda ndiyo itakuwa ya mwisho katika adhabu yangu, hivyo najiandaa kurejea kuipambania timu yangu ili tuweze kubaki ligi kuu.
“Kwa sasa hatupo kwenye nafasi nzuri, hivyo ni lazima tujipange kuhakikisha tunapam­bana katika mechi hizo nane zilizosalia tu­nakuwa salama.”

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic