March 26, 2018


Kiporo cha mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Njombe Mji FC dhidi ya Simba SC kiitachezwa Aprili 3 2018 katika Uwanja wa Sabasaba mjini Njombe.

Kupitia Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema mchezo huo ulioahirishwa ili kuipa nafasi Simba ya kujiandaa na mechi dhidi ya Al Masry katika Kombe la Shirikisho, sasa umepangwa tarehe tajwa hapo juu.

Licha ya mabadiliko hayo, jana uongozi wa Njombe Mji ulilalamikia mabadiliko ya ratiba hiyo wakidai yanawabana kutokana na muingiliano wa mechi za ligi na Kombe la FA.

Ratiba hiyo sasa inaonesha mechi zingine ambazo Simba itacheza baada ya Njombe Mji ambazo ni:-

Mtibwa vs Simba Aprili 9
Lipuli FC vs Simba Aprili 20
Simba vs Yanga Aprili 29

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic