March 11, 2018




Thomas Ulimwengu anasubiria kibali cha kazi ili aweze kuanza kazi ya kuitumikia timu yake mpya iliyopo nchini Bosnia.

Wakati Ulimwengu akisubiri kibali hicho, mwenzake, Farid Mussa anayecheza nchini Hispania, amepandishwa timu ya wakubwa ya Tenerife lakini anakosa nafasi ya kucheza baada ya kutoka kwenye majeraha.

Wawili hao wameitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars ambapo kuitwa kwao kuliibua maswali kwa Watanzania wengi wakihoji imekuaje wameitwa wakati hawachezi kwa muda mrefu.

Meneja wa Ulimwengu, Jamal Kisongo, ameliambia Championi Jumamosi kuwa: “Hakuna tatizo kwa Ulimwengu kuitwa Taifa Stars, hakuna asiyejua kwamba (Ulimwengu) alikuwa na matatizo ambayo ametoka nayo TP Mazembe.

“Mwalimu amezungumza naye na yupo fiti kwani amepata timu huko Bosnia na amekuwa akifanya mazoezi, lakini anashindwa kucheza kutokana na kukosa kibali, mkataba wake huko ni wa muda mfupi.


“Pia ifahamike kwamba hizi mechi ni za kirafiki na si za kimashindano, hivyo mwalimu amemuita ili aone kiwango chake cha sasa.”


Wakati huohuo, taarifa za uhakika kutoka Hispania zinasema, Farid amepandishwa timu ya wakubwa, lakini kwa sasa anashindwa kucheza kutokana na kukosa nafasi hali iliyotokana na kutoka kwenye majeruhi.

1 COMMENTS:

  1. Nafikiria timu ya Taifa ni timu yetu wote watanzania sasa watu wanapotoa maoni yao kuhusiana na hali wanavyoiona kutokana na mwenendo wake wahusika wanapaswa kufahamu yakwamba Watanzania wameshateseka sana na mauzi ya Timu yao ya Taifa. Lakini kama vile haitoshi kila siku zikienda mbele ndio ubabaishaji umekuwa mwingi zaidi kwenye Timu ya Taifa. Sijui yule kocha aliekabidhiwa timu ya Taifa ya Tanzania Bara kule kenya kaishia wapi? Sasa Tanzania inakwenda kucheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa Algeria? Kwa maoni yangu Makocha waliokabidhiwa timu ya Taifa hawana uwezo wa kuipeleka Taifa stars popote pale bado hatupo serious. Hata Simba wameajiri kocha ambae ameshashinda taji la ubingwa wa Africa kwa ngazi ya Timu ya Taifa. Basi Taifa stars ingeajiri kocha angalau aliefanikisha kuipeleka timu yeyote hapa nchini au nje ya nchi raundi ya pili katika mashindano ya Club bingwa Africa. Sasa utaona jinsi gani wahusika wanavyoyachukulia Timu ya Taifa kimzaha mzaha hata ukija kusikia mechi ya Algeria imeota mbawa usije kushangaa wenzetu wanaangalia ubora wa timu wa kucheza wa kucheza nao angalau ubora wa mwalimu uwe na vigezo vinavyoheshimika na kutambulika kimataifa. Hakuna tofauti yeyote kati ya Taifa stars ya Jamali Malinzi na hii ya Sasa katika masuala ya kiufundi kana kwamba bado anaisamamia timu hiyo akiwa gerezani.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic