PATRICK VIEIRA YUKO TAYARI KURITHI NAFASI YA WENGER, HAYA NDIYO AMEYASEMA
Na George Mganga
Nyota wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira, amesema ipo siku atakuja kuifundisha Arsenal japo suala hilo hajaliwekea kipaumbele zaidi.
Arsenal haijawa na kiwango kizuri msimu kufuatia kufanya vibaya katika baadhi ya mechi za ligi.
Vieira ambaye ni Kocha wa New York City FC hivi sasa, amesisitza ana heshima kubwa kwa Wenger kuongelea suala la kuchukua nafasi yake.
"Siwezi kuongelea zaidi suala hilo sababu sina cha kusema, sitaki kumkosea Wenger maana namheshimu na namkubali, lakini ipo siku" amesema Vieira.
Kiwango dhaifu cha Arsenal msimu huu kimeifanya timu hiyo iwe na tofauti ya alama 11 dhidi ya Chelsea iliyo nafasi ya 5 kwenye ligi.
Nafasi pekee ambayo Arsenal wanayo ili kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao, ni kutwaa taji la UEFA Europa League.







0 COMMENTS:
Post a Comment