March 6, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha Simba kimeonesha kweli kimedhamiria kuibuka na ushindi dhidi ya Al Masry SC katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika kesho.

Katika hali isiyo ya kawaida, kikosi hicho kilifanya mazoezi kuanzia majira ya saa moja mpaka mbili usiku wa jana kwenye uwanja wa Boko Vetarani, Dar es Salaam.

Taarifa zinaeleza kuwa wachezaji wapo katika morali nzuri kuelekea mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 12 jioni.

Aidha wachezaji Emmanuel Okwi, John Bocco na Haruna Niyonzima wote walijumuika na wenzao kujifua kuelekea mechi hiyo kubwa.

Simba watafanya mazoezi ya mwisho leo kabla ya kuwavaa Al Masry jioni ya kesho.

1 COMMENTS:

  1. Katika mashindano ambayo yana mechi za nyumbani na ugenini basi timu za Egypt ni mafundi wa kutumia uwanja wa nyumbani kwao kuwamaliza wapinzani wao sasa na sisi timu zetu za Tanzania hasa simba na yanga lazima zijifunze namna ya kupata matokeo ambayo yatawapa wakati mgumu wapinzani wao kuyapindua wakati wa mechi ya marudiano. Miaka nenda rudi timu za Egypt zimekuwa zikizitumia timu zetu kama daraja la kusonga mbele kwenye mashindano ya Africa sasa wakati wa timu zetu kuwa milima baada ya daraja umefika na nnaimani Simba wana uwezo mkubwa wa kuwapa fundisho Almasry kwani mara nyingi wachezaji wamekuwa wakihofia majina ya timu zaidi kuliko uwezo wa timu. Wachezaji wetu uwezo wanao tena mkubwa tatizo wanakosa kujiamini. Kama Simoni Msuva kufika tu Morocco kawa mchezaji tishio. Morocco wapo vizuri hivi sasa kisoka. Kama vile haitoshi Abdi Banda kufika tu Africa kusini kawa mchezaji tegemeo kwenye first eleven na hakuna asiejua ushindani wa ligi ya Africa kusini. Sasa pale simba wapo vijana wengi tu ukiwatupa popote Africa pengine hata nje ya watangara. Kuelekea mchezo wa Simba vs Almasry, wachezaji wa Simba wanatakiwa kuzingatia nidhamu ya kujituma muda wote na kucheza team work yaani kuunganisha nguvu zao kwa kupambana kwa pamoja muda wote wa mchezo. Wiki moja iliyopita rafiki yangu mmisri shabiki wa kujitupa gorofani wa Zamaleki aliniambia unajua kwanini tunakufungeni kila timu zetu zikikutana na timu zenu? Nikamwambia nadhani timu zenu zinauwezo zaidi ya timu zetu akacheka sana akaniambia sio uwezo kwani timu nyingi za Africa zinauwezo zaidi ya timu zao ila timu zao na wachezaji wao huwa wanaekeza kwenye nidhamu zaidi kwenye muda wote wa mchezo na hucheza kwa malengo zaidi. Nidhamu ya mchezaji uwanjani sio kumuogopa referee bali hali ya mchezaji ya kujitambua kuwa yupo uwanjani kuisadia timu yake kupata ushindi kwa nguvu zake zote akisadiana na wenzake na kukosa kwake umakini na kutokujituma kikamilifu ni anguko kwa timu nzima.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic