March 3, 2018


Na George Mganga

Baada ya kuilazimisha Simba sare ya mabao 3-3 katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Ijumaa ya jana, Kocha Msaidizi wa Stand United, Athuman Bila Bilo, amezidi kusema Simba ni ya kawaida.

Akizungumza na Saleh Jembe asubuhi ya leo, Bilo amesema katika mpira siku zote hakuna kudharau timu kwa maana kila upande unakuwa una maandalizi yake ya kupata alama 3, japo halikufanikiwa hilo.

"Unajua katika mpira huwa kuna matokeo matatu, kwa namna tulivyokuwa tumejipanga hayo matokeo tuliyoyapata tunashukuru, Simba ni timu ya kawaida, tushaisahau na sasa akili zetu tunazihamishia kwenye mchezo ujao dhidi ya Tanzania Prisons'' amesema Bilo.

Katika mchezo wa jana, Simba ilikuwa inaruhusu mabao zaidi ya mawili tangu msimu huu wa ligi uanze, huku Aishi Manula akifungwa goli la kwanza la moja kwa moja kwa njia ya kona tangu ajiunge na Simba.

3 COMMENTS:

  1. Makocha wengine ovyoo...badala ya kutueleza walitumia mbinu gani au atupe sababu za kuiona timu ya Simba ni ya kawaida na kama ni ya kawaida basi kwa nini hawakuibuka na ushindi na badala yake wanashangilia sare?
    Sitashangaa kusikia wamefungwa na Prison sababu timu zetu hizi wanakamia timu za Simba na Yanga na mwisho wa ligi wanashuka daraja...mfano ni Toto Africa wako wapi zaidi ya kusikia wanagawana magodoro ya klabu

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kutusimamishia hao wa matopeni nako si jambo dogo. Ha ha haaa!

      Delete
  2. Timu zetu hazina malengo zaidi ya kuzikamia mechi za Simba na Yanga.
    Angesema nini kocha wa stand kama wangeibuka na ushindi?...sare amesema Simba ni ya kawaida...stand ingefungwa Jana kocha angekuambia marefa wamependelea ....mpira wa bongo...wacha tuitane wamatopeni, mikia,vyura,mchangani ili mradi siku inaisha salama

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic