TANZANIA YABURUZA MKIA AFRIKA MASHARIKI KWENYE VIWANGO VYA UBORA WA SOKA DUNIANI
Na George Mganga
Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), limetoa orodha ya Viwango Vya Ubora wa Soka ambapo Tanzania imeshika nafasi ya mwisho ukanda wa Afrika Mashariki.
Uganda inaongoza kwa Afrika Mashariki ikiwa nafasi ya 78 huku Kenya ikiwa nafasi ya pili kwa kushika namba 105, Rwanda ya tatu ikiwa nafasi ya 112 na Tanzania ikiwa mkiani katika nafasi ya 146.
Kwa upande wa Afrika, Tunisia inaongoza kwa kushika nafasi ya 23 huku Germany wakisalia nafasi ya kwanza Duniani na Brazili ikiwa nafasi ya pili.
Kumi bora ya FIFA ipo namna hii
1: GERMANY
2: BRAZIL
3: PORTUGAL
4: ARGENTINA
5: BELGIUM
6 :POLAND
7: SPAIN
8: SWITZERLAND
9: FRANCE
10: CHILE








Kama kungekuwa na sheria ya kushuka daraja kwa timu za taifa basi timu ya Taifa ya Tanzania ingekuwa balaa. Sijui timu yetu ya Taifa ingepangwa daraja gani? Sheria za FIFA za kutaka serikali zisiruhusiwe kutia mkono kwenye vyama mpira sijui kama si hujuma kwa nchi za Africa. Mimi sina wasiwasi hata kidogo yakwamba kama serikali ya Magufuli ingekuwa na dhamana ya maamuzi ya masuala ya mpira wa miguu kwa asilimia mia moja 100% nchini basi mabadiliko tungeshaona katika viongozi wa TFF na hata katika mpira wetu. Ubora wa tunda unategemea zaidi uzima wa Mti. Mtu unapokuwa umechelewa unatakiwa kukimbia. Kufanya mabadiliko ya jambo Dunia ya sasa sio tena ya kusubiri miaka mitano ndio ubadilike . Lakini viongozi wetu wa mpira sio siri wapo very slow kuendana na kasi ya wenzetu. Ni maoni yangu binafsi.
ReplyDelete