March 26, 2018


Wawakilishi wa Barcelona watakutana na wenzao wa Atletico Madrid siku chache zijazo kwa lengo la kukamilisha makubaliano kuhusu uhamisho wa nyota Mfaransa Antoine Griezmann, 27. (Sport - Spain)

Kiungo wa kati wa Liverpool Mjerumani Emre Can, 24, ataihama klabu hiyo bila kulipiwa ada yoyote mwisho wa msimu huku Manchester City na Juventus wakidaiwa kumtaka iwapo klabu yake haitaongeza mshahara wake ambao kwa sasa ni £200,000 kila wiki. (The Sun).

Manchester United wanamtaka beki wa Scotland wa miaka 20 anayechezea klabu ya Celtic Kieran Tierney. (Daily Record)

Inter Milan nao wamewapiku Manchester City na Barcelona na kupata saini ya beki Mholanzi Stefan de Vrij, 26, ambaye atajiunga nao kutoka Lazio bila ada yoyote mwisho wa msimu. (Gazzetta dello Sport - Italy)

Meneja wa zamani wa klabu ya Borussia Dortmund Thomas Tuchel anatarajiwa kuchukua nafasi ya meneja wa sasa wa Arsenal Arsene Wenger mwisho wa msimu. (Kicker - Germany)

Hilo lisipofanyika, Tuchel basi badala ya kwenda Arsenal atajiunga na Paris St-Germain ya Ufaransa, ingawa Chelsea bado wanazisaka huduma zake. (Sportbuzzer - Germany)

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic