April 28, 2018




Na George Mganga

Yanga inashuka dimbani kesho Jumapili ikiwa na vijana wanaopewa nafasi ya kuonesha upinzani mkali dhidi ya kikosi cha Simba kilicho kileleni mwa msimamo wa ligi.

Vijana hao walionolewa na Kocha George Lwandamina, watakuwa chini ya Mkongomani, Mwinyi Zahera ambaye amekabidhiwa majukumu ya kukiongoza kikosi hicho huku akisaidiana na Noel Mwandila.

Lwandamina alikitengeneza kikosi cha Yanga kwa kuwapa nafasi vijana ambao wamekuwa mhimili mkubwa ndani ya timu hiyo hivi sasa.

Yusuph Mhilu, Pius Buswita, Emmanuel Martin, Abdallah Shaibu pia Rafael Daud wamekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza na akiba kwa takribani msimu huu mzima tangu uanze.

Wachezaji hao wanapewa nafasi kubwa ya kucheza katika mchezo dhidi ya watani wao wa jadi Simba, kesho Jumapili.

Mechi hiyo yenye nguvu kubwa hapa nchini na ivutayo hisia kubwa kwa mashabiki wa soka, itafanyika Uwanja wa Taifa kuanzia saa 10 kamili jioni.

5 COMMENTS:

  1. Kwa kikosi cha simba, yanga atasubiri sana

    ReplyDelete
  2. Yanga msimu huu haiwezi kuizuia simba

    ReplyDelete
  3. Simba ya kina ndemla messy mkude ajibu galas walikuwa wadogo zaidiyake na walizicheza

    ReplyDelete
  4. Timu zote zinawachezaji vijana mwandishi uko duna gani

    ReplyDelete
  5. Kwa maana hiyo Simba ina wachezaji wazee, mwandishi uwe makini na matumizi ya maneno

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic