RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA LEO JUMAMOSI YA APRILI 28
Ligi Kuu Tanzania Bara inaendelea Jumamosi ya leo kwa viwanja vitatu nyasi zake kuwaka moto.
Mtibwa sugar itakuwa inaikaribisha Azam FC kwenye Uwanja wake wa nyumbani, Manungu Complex, mjini Morogoro.
Majimaji iliyo katika wakati mgumu wa kuendelea kusalia kwenye ligi msimu huu itakuwa inacheza dhidi ya wazee wa kupapasa Ruvu Shooting katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea.
Mchezo mwingine utapigwa huko mkoani Shinyanga ambapo wenyeji Stand United wameikaribisha Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kambarage mjini humo.
Mechi zote zitaanza saa 10 kamili jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment