May 18, 2018



Wakati kikosi cha Azam kikiwa kinajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons utakaopigwa Mei 20 kwenye Uwanja wa Azam Complex, uongozi wa klabu hiyo waendelea kusisitiza unataka kuwa Makamu Bingwa wa Ligi Kuu msimu huu.

Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano Azam, Jaffer Idd, amesema maandalizi yao kuelekea mechi na Prisons yanaenda vizuri huku akieleza na nia ya kushika nafasi ya pili.

Idd ameeleza kuweka nia hiyo kutokana na bingwa wa ligi kuwa tayari ameshapatikana na sasa wanataka kuweka heshima ya kubaki kwenye nafasi waliyopo ili kuweka heshima.

Uamuzi huo wa Azam kupigania nafasi ya pili unapeleka maombi mabaya Yanga ambao wana mchezo Jumamosi ya wiki hii dhidi ya Mwadui FC huko Shinyanga.

Azam wanaiombea Yanga izidi kuharibu katika mechi zilizosalia ili waweze kumaliza ligi wakiwa kwenye nafasi hiyo ya pili.

Mbali na kucheza na Prisons, mechi nyingine itakayofuata itakuwa ni dhidi ya Yanga, mchezo utakaopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Mei 28 2018 ambapo katika mechi ya mzunguko wa kwanza, Azam ililala kwa mabao 2-0.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic