YANGA YAMALIZANA NA WACHEZAJI WATATU KWA AJILI YA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
Na George Mganga
Uongozi wa klabu ya Yanga kupitia kwa Katibu wake, Charles Boniface Mkwasa, umesema yauari umeshamalizana na wachezaji watatu watakaokuwa na timu hiyo.
Mkwasa ameeleza kuwa watawataja wachezaji hao siku za hivi karibuni ambao watakuwa mhimili mkubwa katika mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika.
Yanga ilipewa nafasi tatu na CAF kusajili wachezaji ili kukipa nguvu kikosi chao ambapo kipo kwenye mashindano hayo ya kimataifa.
Mkwasa amesema hataweza kuwaweka wazi wachezaji akidai wanaweza wakapokonywa na baadhi ya klabu za hapa nchini hivyo wakati ukifika utawataja.
Juzi Jumatano Yanga imekwenda sare na Rayon Sports ya Rwanda ikiwa ni mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho.
Wakati huo timu hiyo ipo njiani hivi sasa kuelekea Shinyanga kwa ajili ya mechi ya ligi dhidi ya Mwadui FC itakayopigwa Uwanja wa CCM Kambarage.
Kutoka Spoti Leo - Radio One.
Ushauri wanu ulikuwa kwa Pappy Kambale, Lubinda Mumbia na Kotinyo....Au Mohamed Rashid na Mpepo kutoka Prison...hii nilitoa kutokana na mazoeano na aina ya mpira wa mfanano wa timu zetu kwenye eneo la ushambuliaji. nataka nione wapi Yanga wamewatoa hao watatu..nikikosa kwenye hilo nitajua
ReplyDeleteSi hapa, leo yanga imefika hadi kuwa na woga wa kuwataja wachezaji wanaotaka kuwasajili kwa hoja wanaogopa Ukowapi ubabe wa yanga wa kuwanyanyasa simba kwa kuwachukuwa nyota wao kila wanapoamuwa kuwachukuwa. Ubata wa yanga ni kuwa waliondokea kumfanya Manji kama mama kwa mtoto wake mchanga ambaye ndie muhili wa timu na ulipotenguka ni ikawa basi tena.
ReplyDeleteMbona hata samba inamtegemea mtu mmoja tu.
DeleteKutokana maneno ya mkwasa ndio mana lipuli walikuwa na wasiwasi na mchezajiwao kumbe hawana nia ya kuazimwaila walitaka kymsajiri kupitia fimbo njia ya mkato
ReplyDeleteDuuuuuh!!!!!! Kumbe Lipuli walikuwa sahihi kwa ajili ya kugomea kumtoa mchezaji wao. Sasa Mkwasa unafikia hatua unakataa kutambulisha wachezaji wa aina gani? Sasa ushauri mtaupata wapi jamani?
ReplyDeleteProtas-Iringa
mpira hauchezwi magazetini
ReplyDelete