May 27, 2018


Na George Mganga

Shirikisho la Soka Tanzania Bara kupitia Bodi ya Ligi, limesema kuwa litazifuatilia kwa jicho la tatu mechi kadhaa za kuhitimisha safari Ligi Kuu kesho ili kuepusha upangaji wa matokeo.

Ligi hiyo ambayo bingwa wake tayari ameshapatikana, Simba SC, inafikia tamati hapo kesho ambapo jumla ya mechi nane (8) zitapigwa katika viwanja tofauti hapa nchini.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Ligi, Boniface Wambura, amesema kuwa mechi ambazo zitahusisha timu zinazojikwamua kushuka daraja zitatazamwa kwa kina ili kuepusha suala la upangaji wa matokeo.

Wambura amesema wataitazama zaidi mechi baina ya Simba na Majimaji FC itakayopigwa kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea ambapo Majimaji inatakiwa kushinda huku ikiiombea Ndanda FC ipoteze dhidi ya Stand United ikwepe kushuka daraja.

Mbali na mechi hiyo, nyingine itakayofuatiliwa zaidi ni ile ya Yanga dhidi ya Azam FC itakayopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam majira ya saa 10 jioni.

Vilevile mechi nyingine ni Ndanda FC itakayokuwa nyumbani kuikaribisha Stand United ya mjini Shinyanga ambapo wenyeji wa mechi hiyo watahitaji matokeo ya sare ili waweze kusalia kwenye ligi msimu ujao.

Timu hizo zote zinawania kumaliza ligi zikiwa nafasi ya pili, Yanga atapata nafasi hiyo endapo ataibuka na ushindi wa aina yoyote ilihali Azam wanapaswa kwenda sare ili kusalia kwenye nafasi ya pili.

Yanga wana pointi 52 wakati Azam ana 55 hivyo Yanga ataipiku Azam kuishusha mpaka nafasi ya tatu endapo atashinda kwani watalingana alama lakini atakuwa juu kutokana na wingi wa mabao ya kufunga.

4 COMMENTS:

  1. Hpa anaefuatiliwa ni yanga huko simba hakuna jipya tff ni simba Tupu waxtupumbaze maji maji anabebwa kexho

    ReplyDelete
  2. Yanga akishinda ni Wa pili kinachoangaliwa si magoli ni matokeo ya mechi zao nani? Alipoteza.

    Waandishi julisheni ukweli ulio katika kanuni sio kukariri.

    Hili lilisemwa mapema timu zikilingana pointi kinachoangaliwa kwanza matokeo baina yao.

    ReplyDelete
  3. Yanga akishinda ni Wa pili kinachoangaliwa si magoli ni matokeo ya mechi zao nani? Alipoteza.

    Waandishi julisheni ukweli ulio katika kanuni sio kukariri.

    Hili lilisemwa mapema timu zikilingana pointi kinachoangaliwa kwanza matokeo baina yao.

    ReplyDelete
  4. Hiyo kanuni YA kumpata mshindi kwani kuangalia Nani kamfunga mwenzake imeanza kutumika lini. Maana msimu ulomalizika simba na yanga walilingana pointi lakini yanga akabeba ubingwa kwa tofauti YA magoli ili Hali simba alimfunga yanga walivyokutana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic