May 27, 2018





Pamoja na kuenea kwa taarifa kwa Mjumbe wa Kamati wa Utendaji ya Yanga, Salum Mkemi amejiuzulu, imeelezwa bado anaendelea kuitumikia klabu hiyo.

Mmoja wa viongozi wa Yanga, ameiambia SALEHJEMBE kwamba pamoja na ukimya lakini Mkemi bado yuko Yanga.

“Bado tupo na Mkemi na tunaendelea vizuri kabisa,” alieleza.

“Huenda watu wamesikia wakaamini, maana  niliposikia nikazungumza naye na kasema hana huo mpango.”

Mkemi ni kati ya viongozi vijana wanaoiongoza Yanga na wamekuwa katika wakati mgumu kutokana na klabu hiyo kuandamwa na ukata.

Baadhi ya wanachama na mashabiki wamekuwa wakishinikiza ajiuzulu jambo ambalo yeye bado hajapatikana kulizungumzia.

3 COMMENTS:

  1. I would loke to remind Yanga leadership that, falling down is not a defeat, but a defeat is to remain where you have fallen. Patience is bitter, but its fruits are sweet

    ReplyDelete
  2. Muungwana yeyote wakati ukifika anajiuzulu ukiona hivyo bado wakati haujafika endelea na kazi.

    ReplyDelete
  3. Huyo jamaa hana msaada kwa klabu ni moja ya mizigo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic