Mtanzania, Mbwana Samatta ameonyesha kuwa sasa kweli amepona baada ya kuendelea kucheka na nyavu huko Ubelgiji.
Samatta ameifungia timu yake ya KRC Genk bao la kwanza katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Zulte-Waregen.
Mshambuliaji huyo mwenye kasi, alipokea pasi ya Leandro Trossard katika dakika ya 18 na kuandika bao hilo la kwanza.
Sakika 10 baadaye, yaani dakika ya 28, Jere Uronen aliandika bao la pili kwa Genk akiunganisha pasi ya Alejandro Pozuelo.
Baada ya Ligi Kuu ya Ubeligiji kwisha, sasa Samatta anatarajia kurejea nchini na kucheza mechi ya kuchangia wanafunzi.
Mechi hiyo itakuwa kati ya Rafiki wa Samatta dhidi ya Rafiki wa Ali Kiba, msanii maarufu nchini wa muziki.
0 COMMENTS:
Post a Comment