Real Madrid imeitwanga Liverpool kwa jumla ya mabao 3-1 na kubeba ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya 13.
Lakini taarifa ya kwamba Mohamed Salah huenda akakosa michuano ya Kombe la Dunia nchini Russia ndiyo zimezua mshituko mkubwa.
Taarifa hizo zimezua mshituko kwa kuwa Salah aliumia baada ya kuangushwa na nahodha wa Madrid Sergio Ramos. Akalazimika kutolewa kipindi cha kwanza.
Lakini mshituko hasa kwa mashabiki wa soka wa Misri, ambao wameanza kutaka kujua imekuwaje kwamba anaweza kukosa Kombe la Dunia.
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp akihojiwa na waandishi wa habari baada ya mechi hiyo, amesema kuna hofu hiyo kwa kiasi kikubwa kwa kuwa inaonekana amepata madhara makubwa katika bega lake.
Hata hivyo akasisitiza, lazima wapate majibu baada ya vipimo vya X Ray na baada ya hapo, watajua kama kuna uwezekano wa kumsaidia matibabu ili aitumikie Misri.
Mashabiki kupitia mitandao nchini Misri wamekuwa wakivurumisha maneno makali kwa Sergio Ramos na wengine wakitaka kujua uhakika kuhusiana na hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment