May 27, 2018


Na George Mganga

Kikosi cha klabu ya Simba kimewasili salama mijini Songea kwa ajili ya mchezo wa ligi dhidi ya Majimaji FC utakaopigwa kesho Jumatatu.

Simba ambao ni mabingwa wapya wa VPL msimu huu wamewasili Songea Jumamosi ya jana huku wakiwa na wachezaji wengi wa kikosi cha pili.

Wekundu hao wa Msimbazi wameamua kupeleka wachezaji wengi wa kikosi cha pili huku wengine wakisalia Dar es Salaam kuanza maandalizi ya kujiandaa na michuano ya SportPesa Supar Cup.

Michuano hiyo inatarajia kuanza mwezi Juni jijini Nairobi Kenya itakayoshirikisha timu zote ambazo zinazodhaminiwa na Kampuni hiyo ya michezo ya bahati nasibu.

Kuelekea mchezo na Majimaji, Simba wametamba kupambana ili waweze kupata alama tatu muhimu kwa ajili ya kuendelea kuweka heshima kwenye ligi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic