May 10, 2018





DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, Prisons wanafanya shambulizi jingine lakini krosi ya Mpepo inatoka nje
KADI Dk 86, Kakolanya analambwa kadi ya njano kwa kuzozana na mwamuzi
GOOOOOOOOO Dk 85, Salum Bosco aliyeingia dakika chache zilizopita anaandika bao la pili kwa Prisons
SUB Dk 81 Yanga wanamuingiza Yusuf Selemenani na kumtoa Akilimali, Paul Geofrey anatoka kuchukua nafasi ya Amissi Tambwe 
Dk 80 Kamusoko anaachia mkwaju mzuri lakini anamlenga kipa
Dk 78, taratibu Yanga wanaanza kupanga mashambulizi vizuri
Dk 74, mpira wa adhabi, Kakolanya yuko makini anatoka na kudaka vizuri kabisa
Dk 72, Mpepo tena, anagongeana vizuri na Mpalile na kuachia mkwaju mkali hapa, goal kickKADI Dk 69, Jumanne El Fadhil wa Prisons analambwa kadi ya njano kwa mchezo wa kibabe 



Dk 65 Mpepo anapiga krosi safi hapa lakini Mohammed Rashid na kipa Kakolanya, anashindwa kulenga

SUB Dk 62 Vedastus Mwihambi anaingia upande wa Prisons kuchukua nafasi ya Mwasote
Dk 60, Ismail wa Prisons anaachia krosi safi kabisa lakini Kakolanya yuko makini
GOOOOOOOO  Dk 57, Mpepo anaukwamisha upande wa kushoto mwa Kakolanya naye anaufuata lakini wapii...
PENAAAAAAATI Dk 56, mwamuzi anasema Kamusoko aliunawa ule mpira
Dk 55 MOhammed anaingia kwa kasi, anapiga krosi matata hapa, lakini Kakolanya yuko vizuri
Dk 53 Mpepo anaachia mkwaju, unaokolewa na Yanga sasa wanamiliki



Dk 53, milango bado ni migumu lakini Yanga wanaonekana wametulia hata kuliko walivyotarajiwa na wanacheza soka safi la ushindani

Dk 50, Mpepo anajaribu tena lakini Kakolanya yuko vizuri kabisa, anadaka
Dk 48 kona inachongwa vizuri, Matheo anajitwika lakini kipa yuko makini
Dk 47 Yanga wanafanya shambulizi zuri hapa, Nkomola anaachia mkwaju inaokolewa na kuwa kona 
Dk 46 Mechi imeanza kwa kasi na Prisons inaonekana kuanza kwa kasi 

MAPUMZIKO


DAKIKA 2 ZA NYONGEZA

Dk 45, krosi maridadi, Nkomola anaachia kichwa safi na mpira unapira sentimeta chache nje ya lango la Yanga
Dk 42, Mohammed Rashid na Mpepo wanagongeana vizuri ndani ya lango la Yanga lakini wanapoteza nafasi
Dk 39, Prisons tena wanaingia kwenye lango la Yanga na kuachia mkwaju mkali kabisa, goal kick



Dk 38, Mpepo tena pembeni anaachia mkwaju mkali lakini hakulenga lango

Dk 36, mpira kidogo umetawaliwa na ubabe kutoka kila upande na mwamuzi analazimika kuamua
Dk 34 kona ya nne ya Prisons inachongwa, El Fadhili anacheza faulo
Dk 33 Mpepo anaingia vizuri, Juma Abdul anamzuia na kuwa kona ya tano ya Prisons, inachongwa, hakuna kitu, kona tena
Dk 30 Prisons wanapata kona nyingine, hata hivyo Ninja yuko kamili, anaondosha kwa kichwa na mwamuzi anasema amefanyiwamadhambi
Dk 27, al manusura Yanga ipitie bao kupitia Matheo Anthony lakini kipa anatokea na kudaka na mwamuzi anasema ni offside


Dk 24, kidogo inaonekana matumizi ya nguvu yanachukua nafasi kubwa na mara kadhaa, mwamuzi analazimika kuwaonya wachezaiji

Dk 20, Yanga wanajibu shambulizi, Prisons wako makini wanaokoa na kuwa kona ya pili ya Yanga, mwamuzi anasema ni faulo baada ya kipa kufanyiwa madhambi ingawa inaonekana alipoukopa mpira akateleza
Dk 20 kona inachongwa hapa, Mpepo anapiga kichwa akiwa peke yake, mpura unapita juu kidogo ya lango la Yanga, goal kick
Dk 18 kona ya ya Prisons inachongwa hapa, YAnga wanaokoa, shuti wanajichanganya, kona nyingine
Dk 18, Priosns wanapata kona ya kwanza, inachongwa vizuri na Mpepo anaachia mkwaju, Kakolanya anaokoa na kuwa kona nyingine
Dk 17, Asukile anaachia mkwaju mkali kabisa hapa lakini unatoka sentimeta chache pembeni ya lango la Yanga
Dk 15, bado mpira unachezwa katikati lakini taratibu timu zinaanza kufunguka


Dk 13 sasa, Yanga wanaonekana kucharuka na Akilimali anaonekana kuitikisa beki ya Prisons

Dk 10, Eliuta anaamua kujaribu kutoka mbali lakini hakulenga lango
Dk 8 sasa, bado mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mipango mingi ya mashambulizi matata
Dk 4, mabeki wa Yanga wanajichanganya na kipa, lakini Ninja anaosha, unakuwa wa kurushwa
Dk 2, Yanga wanaonekana kumiliki mpira vizuri zaidi katikati ya uwanja
Dk 1, Yanga wanafanya shambulizi na Prisons wanatoa na kuwa kona, inachongwa na Akilimali, kichwa safi, goal kick
Dk 1, Prisons inakuwa ya kwanza kufika katika lango la Yanga, lakini Kakolanya anaonekana yuko makini


3 COMMENTS:

  1. Hilo tulitarajia tu

    ReplyDelete
  2. Hilo gepu la zaidi ya 30 minutes of updates zinatia shaka kwa mechi inayourushwa 'live'. Lakini inakubalika kwa personal blogs.

    Anyway, safari njema kuelekea ligi daraja la pili. Tutawamiiisss sana katika anga za kimataifa, ... ila ni mapenzi ya Mungu. Masikini Yaaangaaa, ... Mhhh!!

    ReplyDelete
  3. Inatia UCHUNGUUU

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic