MANARA AJITOLEA KUWALIPIA VIINGILIO WASIOKUWA NACHO KESHO, AWAKARIBISHA YANGA KUPOKEA UBINGWA SIMBA
Na George Mganga
Kuelekea mechi ya Simba SC dhidi ya Kagera Sugar, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa klabu ya Simba, Haji Manara, amesema atajitolea kuwalipia mashabiki kiingilio.
Manara amefikia uamuzi kutokana na hitaji lake la kuwataka wanachama na wapenzi wa Simba kujitokeza kwa wingi katika mechi hiyo ambayo itahudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli.
Akizungumza na Radio EFM kupitia Sports HQ, Manara ameeleza kuwa kwa wale baadhi watakaokuwa hawana fedha za kiingilio, atakuwepo getini na bunda le fedha kuwapatia Tshs 2000 kwa kila mmoja.
Mbali na kujitolea kiingilio, Manara amewaomba watani zake wa jadi Yanga kuja kwa wingi Uwanjani hata kama watakuja kuzomea huku akieleza kuwa hiyo ndiyo burudani ya soka.
Mechi hiyo dhidi ya Kagera itaenda sambamba na Simba kukabidhiwa kombe la ligi waliloshinda msimu huu ambapo Rais Magufuli ndiye atakayewakabidhi taji hilo.
Duuuh, ... ndugu yangu SANDE punguza spidi na ukumbuke kubakiza maneno wasije wakanywa thumuu, ... kumbuka kuwa hao mayebo wetu tunawahitaji msimu ujao na siku zote ili kunogesha Vadakom Primiyaaa Ligyi.
ReplyDeleteTeheh heh hehhhhh
Soka LA bongo bwana WA jangwani wamechukua mara3 mfululizo hakuwa na kelele, na ndo timu inayoongoza kupiga hatrick vpl nahs kwa rekodi ya toka 91 hakuna timu iloweza WA jangwani wamepiga hatrick mara 3,zeemba ni sawa na watoto wanashangilia kupewa pipi
ReplyDelete