May 5, 2018


Baada ya kuwasili nchini akiwa na takribani siku nne sasa, kiungo wa Simba, Mnyarwanda, Haruna Niyonzima, ameelezea furaha yake kufuatia timu yake kuifunga Yanga kwenye mchezo wa ligi, Jumapili iliyopita.

Niyonzima ambaye alikosekana baada ya kusafiri kurejea kwao kuhudhuria msiba wa dada yake aliyefariki, amesema amefurahi Simba kushinda huku akiamini itaweza kutwaa ubingwa.

Mbali na furaha hiyo, mchezaji huyo amesema kuelekea mechi na Ndada itakuwa ni fainali kwa kuwa kila mechi wao wanazichukulia hivyo ili waweze kubeba ubingwa ambao haujapatikana Simba kwa muda mrefu.

Simba itakuwa inaingia kibaruani kesho kuikabili Ndanda FC kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam kuanzia saa 10 kamili jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic