Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wamealikwa bungeni mjini Dodoma kwa mwaliko wa Spika wa bunge hilo, Job Ndugai.
Simba walihudhuria bungeni na kila mmoja alikuwa na pozi lake, kama unavyojua, wachezaji hawajazoea kukaa muda mwingi, hayo ni mambo ya kiofisi, wao wanapambana uwanjani.
Pamoja na yote, pozi la kuvutia zaidi lilikuwa ni la Msemaji wao, Haji Manara ambaye aina yake ya ukaaji, ilionekana kuwavutia wengi.
Manara alionekana kukaa kama mtu aliyekuwa anataka kupaa hivi, ukaaji wa maringo na kujiamini, hali iliyokuwa ikitafsiri furaha yake ya ubingwa.
Kila Simba ilipofeli kupata ubingwa, Manara amekuwa ndiye mtu anayeandamwa zaidi na watani wake wa jadi, Yanga kwa kuwa amekuwa akiwachemsha mfululizo.
Lakini tokea Simba imechukua ubingwa, inaonekana wazi Manara ana ahueni kubwa na hata muondoko wake, kiasi umeongezeka mikogo.
Amekuwa akisisitiza kwamba atazungumza sana na Yanga wajiandaa kwa kuwa Simba imechukua ubingwa unaostahili, maana ni ubingwa wa halali maana kabla ya mechi tatu, tayari walibeba ubingwa na si suala la kutofautiana kwa mabao ya kufunga na kufungwa.








How could you mention Manara without mentioning Simba or Simba without Manara the Great
ReplyDelete