May 4, 2018



Na George Mganga

Kiongozi wa zamani wa klabu ya Simba, Mwina Kaduguda, ameitaka klabu ya Simba kuzingatia mambo yafuatayo kama itautwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara ili kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.

Kaduguda maarufu kwa jina la Simba wa Yuda, amesema kama timu hiyo itauchukua ubingwa, tayari itakuwa ina tiketi ya moja kwa moja kushiriki mashindano ya kimataifa haswa Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza kupitia Radio One, Katibu huyo wa zamani ameitaka Simba kuanza mipango ya mapema kwa ajili ya kukiweka kwenye makali kikosi chake ikiwemo kufanya usajili wa wachezaji wakali ili kukiboresha zaidi.

Aidha, Kaduguda ameeleza kuwa ni vema Simba wawe wanatuma watu maalum kwenda kuzichunguza timu pinzani pale wanapopangiwa nazo mapema kabla ya kuvaana nazo, akidai kuwa itawasaidia kuwarahisishia mipango ya kupata matokeo.

Kiongozi huyo ameshauri Simba wasajili wachezaji wenye levo sawa ya mashindano na si sawa na wale wanaopambana kuifunga Yanga pekee au Stand United, jambo ambalo si sawa.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic