May 14, 2018



Timu ya watoto wa kike wanaoishi katika mazingira magumu kutoka nchini Tanzania, imeifunga timu ya watoto kama hao kutoka nchini Marekani, jumla ya mabao 5-0 katika mashindano ya Street Children World Cup na kufanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali.

Katika mashindano hayo yaliyoandaliwa na Shirika la Street Child United, timu ya wasichana ya Tanzania imefanikiwa kutinga hatua hiyo ya nusu fainali, ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja naikiwa haihafungwa goli hata moja, na kuweka rekodi ya kipekee.

Mchezo wa timu ya Tanzania dhidi ya Marekani, umefanyika katika Uwanja wa Timu kubwa ya Soka ya Lokomotive Moscow jijini Moscow nchini Urusi ambapo mshambuliaji wa Tanzania, Yasinta Peter anaongoza kwa kufunga magoli mengi zaidi, ambapo mpaka sasa amezifumania nyavu mara 5.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic