July 1, 2018


Unaambiwa hivi ile ishu ya Deus Kaseke kwamba anakwenda Sauzi ni geresha tu, kama mambo yatakwenda sawa basi wikiendi hii kiungo huyo wa Singida United, anatarajiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja Jangwani.

Kaseke ambaye alichezea Yanga msimu miwili iliyopita kabla ya msimu wa 2017/18 kujiunga na Singida United. Chanzo makini kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa Kaseke ilikuwa asaini mkataba juzi Ijumaa lakini kuna vitu vikashindikana katika makubaliano yao hivyo wikiendi hii anatarajiwa kusaini kandarasi hiyo.

Kiliongeza kuwa Kaseke alikuwa anaidai Singida fedha yake ya usajili uliopita hivyo Yanga wameingilia na sasa watamlipa fedha anayoidai kutoka singida kisha watamungozea kiasi kingine ili asaini mkataba haraka.

Pia Yanga ililazimika kumzuia nyota huyo kucheza mechi ya juzi ya Kombe la Kagame dhidi ya APR ya Rwanda kwa hofu ataumia hivyo kushindwa kumtumia kwenye michuano yake ya kimataifa ambapo wanashiriki Kombe la Shirikisho.

Alipotafutwa Kaseka alisema: “Nipo kwenye mazungumzo na Yanga na yanakwenda vizuri muda wowote nitasaini mkataba.” Awali baada ya Kocha Hans Pluijm kuondoka Singida na kujiunga na Azam FC, Kaseke ilidaiwa kwamba hajaongeza mkataba atakwenda Afrika Kusini.

4 COMMENTS:

  1. Naona kama ni kiki za kutafuta mkataba Msimbazi kwani Kaseke kwenda Yanga sio issue hata kidogo alishamuwepo hapo.

    ReplyDelete
  2. Sasa ivi wanaitumia Yanga tu ili wapate ulaji simba .....wamsajili na huyo ahaa ahaa ahaa

    ReplyDelete
  3. Unafurahisha sanaa mwandishi uchwaraa wewe,yote hayo ñi kuwapigiaa chapuo simba basi ukweli ni kwamba yanga itaendelea kubaki yanga na Leo no kutufanya sisi wanayanga tuwaone viongozi wetu sio bora BT mumeshindwa kwahilo

    ReplyDelete
  4. Unafurahisha sanaa mwandishi uchwaraa wewe,yote hayo ñi kuwapigiaa chapuo simba basi ukweli ni kwamba yanga itaendelea kubaki yanga na Leo no kutufanya sisi wanayanga tuwaone viongozi wetu sio bora BT mumeshindwa kwahilo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic