June 28, 2018


Ikiwa imesalia siku moja pekee kuelekea kuanza kwa michuano ya KAGAME itakayokuwa inachezewa jijini Dar es Salaam, uongozi Azam umetaja wachezaji itakaowakosa.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu hiyo, Jaffer Idd Maganga, amesema kikosi chao kitakosa huduma ya wachezaji Tafadzwa Kutinyu, Donald Ngoma na Yakubu Mohammed.

Maganga ameeleza sababu za kukosekana kwa wachezaji Kuntinyu na Mohammed ni mapumziko ambayo waliomba wapewe hivyo watarejea siku kadhaa kabla ya ligi kuanza.

Aidha, Kocha Hans van der Plujim naye hatokuwepo kwenye benchi la ufundi la Azam wakati wa michuano hiyo kutokana na likizo yake kuwa ndefu baada ya kurejea kwao Uholanzi kwa mapumziko pia.

Mashindano hayo ya KAGAME yataanza kesho Juni 29 ambapo bingwa mtetezi Azam FC ataanza kucheza kibarua chake dhidi ya Kator FC kwenye wake wake wa nyumbani, Chamaz Complex.

1 COMMENTS:

  1. Lazima kuwepo sababu,sasa Huyo ngoma amepewa mapumziko ya nini?ha ha ha ha semeni ukweli NGOMA bado ina pancha,kutinyu nae hakijaeleweka.mnajifanya kujitetea eti mapumziko Kwa kazi gani haswa waliotoka kuifanya.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic