June 28, 2018


Na George Mganga

Aliyewahi kuwa mwenyekiti wa klabu ya Simba, Hassan Dalali, amesema kuondoka kwa Yanga katika mashindano ya KAGAME kumeondoa msisimko mkubwa.

Dalali amesema hayo kutokana na timu hizo zinapokuwa pamoja katika mashindano yoyote hapa nchini na nje, huleta msisimko mkubwa tofauti na timu zingine ambazo hazina idadi kubwa ya mashabiki.

Mwenyekiti huyo wa zamani amefunguka na kueleza kama Yanga wasingeweza kujitoa kungekuwa na hamasa kubwa ya mashindano sababu timu hizo zinapokutana kunakuwa na tambo nyingi za aina yake.

Aidha, Dalali ameeleza kitendo cha Yanga kujitoa ni kutokana na Simba kufanya usajili wa kutisha na akisema wameingia mitini wakiogopa kufungwa bao sita.

Dalali anaamini kuwa Yanga wamejitoa sababu ya Simba kuwa imara hivi na aina ya wachezaji ambao inasajili na akidai kuwa wamekimbia mashindano kukwepa aibu.

"Hawa Yanga wamekimbia tu mashindano, laiti kama wangekuwepo wangeweza kupigwa bao sita. Usajili tunaoufanya hivi sasa ni wa kutisha, wameogopa tu, hakuna kingine" amesema.

1 COMMENTS:

  1. waambie wandaaji wa mashindano haya kuwa Yanga huwa haishiriki mabonanza. Bao sita kawafungeni washiriki wenzenu wa mabonanza

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic