June 28, 2018


Michuano ya Kombe la Dunia Urusi inaendelea tena leo ambapo Afrika itakuwa inawakilishwa na timu mbili.

Senegal ambayo ilikubali kwenda sare ya mabao 2-2 na Japana katika mchezo uliopita itakuwa inakipiga dhidi ya Colombia leo kwenye mchezo wa kundi H, mchezo ukianza saa 11 jioni.

Ili Senegal iweze kusonga mbele inahitaji kufanya vizuri mchezo wa leo huku ikiombea Japan iweze kupoteza dhidi ya Poland au mechi iende sare.

Vilevile Tunisia ambao tayari wameshayaaga mashindano watakuwa wanacheza dhidi ya Panama kwenye mchezo kundi G, mechi ikianza saa 3 kamili usiku.

Michez mingine itakuwa baina ya England dhidi ya Belgium kutoka kundi G kuanzia saa 3 kamili usiku huku Japana na Poland nao wakicheza saa 11 jioni.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic