BAADA YA KUISADIA BRAZIL KUITANDIKA COSTA RICA, COUTINHO ABEBA TUZO YA MCHEZAJI BORA
Kiungo mshambuliaji wa Brazil, Philippe Coutinho ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa mechi dhidi ya Costa Rica leo.
Coutinho ametwa tuzo hiyo ambayo ni ya pili katika michuano hii baada ya kuifungia Brazil kupata bao la kwanza na la pili akimtengenezea Neymar.
Coutinho anakuwa anajiwekea rekodi yake ndani ya kikosi cha Brazil katika michuano ya Kombe la Dunia mwaka huu akiwa mchezaji pekee kutwaa tuzo hiyo.
Kiungo huyo anayeichezea FC. Barcelona amekuwa na mchango mkubwa katika mechi mbili ambazo Brazil imecheza kwenye kundi E.
0 COMMENTS:
Post a Comment