June 22, 2018


Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Simba, Haji Manara, amewashauri Yanga kuachana na dhana ya kumtegemea Yusuf Manji pekee kwa lengo la kuisaidia klabu yao.

Manara ameandika hayo kupitia ukurasa wake wa Instagram akiwataka Yanga wajikite katika kufanya mfumo wa mabadiliko ya uendeshwaji wa klabu badala ya kuendelea kumlilia Manji ili aendelee kuwa Mwenyekiti wa klabu.

Manara ameeleza kuwa Yanga wanapaswa kufanya kile Simba wameshakitekeleza kwa sasa ili kuendeana na mfumo mpya ambao hautoweza kumtegemea mtu pekee yake badala yake uwekezaji utachukua nafasi.

Hali ni tete sana, leo Yanga inategemea mtu badala ya mfumo. Simba haijawahi kumpigia magoti mtu na ndiyo maana tumebadili muundo wa klabu, msipobadili muundo na mfumo na kuamini mtu ndiyo kila kitu ipo siku mtadhalilika" ameandika Manara.


Andiko hilo fupi limekuja mara baada ya Yanga kupitia Mkutano wake Mkuu uliofanyika hivi karibuni kupinga barua ya Manji iliyoomba ajizulu na wanachama wote waliohudhuria mkutano wakitaka aendelee kuwa Mwenyekiti.

2 COMMENTS:

  1. Kwa mara ya kwanza namshuhudia Manara akitoa ushauri wenye tija kwa Yanga. Hats hivyo we endelea na club yako

    ReplyDelete
  2. Huyu mtu hawezi kuizungumzia masuala ya timu bila kuzungumzia masuala ya timu ya wananchi? hatupumui?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic