Beki wa zamani wa Azam FC, Pascal Wawa amemuambia rafiki yake wa karibu kuwa lazima atasajiliwa Simba.
Wawa amemuambia rafiki yake huyo kwamba ana uhakika atasajiliwa Simba kwa kuwa atauvuka mtihani aliopewa.
"Uongozi wa Simba umemtaka kuonyesha kiwango katika michuano ya Kombe la Kagame inayoanza mwishoni mwa wiki.
"Wawa anaonekana anajiamini sana, amesema kwa mtihani huo anajiamini atasajiliwa," alisema rafiki yake huyo ambaye hakutaka kutajwa.
Lakini mmoja wa viongozi wa Simba, alisisitiza kwamba kama atafuzu kwa kuonyesha kiwango sahihi katika michuano ya Kagame, basi watamsaini.
Tayari Wawa amekuwa akijifua na kikosi cha Simba tayari kwa ajili ya michuano hiyo ya Kombe la Kagame.
0 COMMENTS:
Post a Comment