BANDA (KUSHOTO) AKIWA NA SALEHJEMBE WALIPOKUTANA NCHINI AFRIKA KUSINI HIVI KARIBUNI. |
Beki wa Baroka FC ya Afrika Kusini, Abdi Banda amemaliza likizo yake na kurejea kazini.
Tayari Banda ameanza kazi rasmi kwa ajili ya msimu ujao baada ya mapumziko ya wiki mbili hapa nchini.
“Sasa niko Afrika Kusini kazini, tayari nimeanza kazi baada ya likizo,” alisema Banda akionyesha yuko makini na kazi yake.
Banda raia wa Tanzania amekuwa na mafanikio katika msimu uliopita katika Ligi Kuu ya Afrika Kusini.
Baadhi ya timu zimekuwa zikimuwania lakini yeye amekuwa akisisitiza kazi yake ni kucheza mpira na suala la kusaka timu anamuachia wakala wake.
0 COMMENTS:
Post a Comment