Pamoja na kocha wa zamani wa Singida United, Hans Pluijm kutimkia Azam FC, lakini ameendelea kutumika katika usajili wa timu yake hiyo ya zamani kutokana na ripoti aliyoikabidhi.
Meneja wa timu ya Singida United, Festo Sanga amesema kuwa, usajili kwa timu yao unazingatia ripoti ambayo waliachiwa na Plujim baada ya kuifundisha timu hiyo kabla ya kutimkia Azam.
“Tunafanya usajili makini ambao utakuwa na manufaa kwa mchezaji na timu ,kikubwa ambacho tunazingatia ni ripoti ambayo ilitolewa na kocha aliyepita (Hans Pluijm) kwani alikabidhi mapendekezo yake na pia tunatumia na mapendekezo ya mwalimu mpya katika kusajili.
“Kikubwa tunachoangalia sio kusajili tu mchezaji ndani ya timu kisha asipate nafasi ya kucheza tunatazama mahitaji ya timu pamoja na nafasi ya mchezaji ndani ya timu,pia tunaandaa kikosi ambacho kitakuwa na muda mrefu ndani ya timu ndio maana tunasajili kuanzia miaka miwili na kuendelea kwenye mikataba,” alisema Sanga.
Wachezaji ambao wamesajiliwa na Singida United hadi sasa ni pamoja na Habibu Kiyombo, Tiber John, Eliuter Mpepo, Kazungu Mashauri, Diaby Amara ikiwa ni wachezaji wa mwanzo baada ya kufunguliwa kwa dirisha la usajili.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment