June 20, 2018


Baada ya Senegal ya Afrika kuitwanga Poland ya Ulaya kwa mabao 2-1, inaonekana suala la bao la pili lililofungwa na Mbaye Niang ndiyo limekuwa mjadala mkubwa katika nchi za Ulaya.

Nchi nyingi za Ulaya wamekuwa wakijadili kuhusiana na mfungaji kwamba alikuwa ameotea.

Niang alikuwa nje anatibiwa, wakati anaingia Senegal ilikuwa inashambulia naye akakimbia na kuuwahi mpira kabla ya kufunga.

Jambo hilo linaonekana kuwakera sana mashabiki wa soka wa Poland na hats Ulaya nzima.

Vyombo via habari vimewapa nafasi mashabiki kujadili suala hilo kwa kina kwa lengo la kupata jibu huku wengi wakilalia kutaka kuonyesha ilikuwa ni offside.


Haya hivyo, kwa sasa soka inachezeshwa na waamuzi zaidi ya watano, wengine wakiwa kwenye running, hali inayoonyesha, bao hilo lilikuwa bomba tu.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic