Mshambuliaji, Obrey Chirwa raia wa Zambia, amefanikiwa kujiunga na Ismailia inyoshiriki Ligi Kuu ya Misri kwa mkataba ambao umefanywa kuwa ni wa siri.
Chirwa ambaye ameitumikia Yanga kwa misimu miwili kabla ya mkataba wake kumalizika hivi karibuni, ametimkia kwenye timu hiyo kutokana na kushindwana na Yanga katika kuongeza mkataba.
Mzambia huyo alijiunga na Yanga mwanzoni mwa msimu wa 2016/17, akitokea FC Platinium ya Zimbabwe kwa ada ya uhamisho wa Sh milioni 240.
Chanzo kutoka Misri kinasema kuwa, mchezaji huyo alikuwa nchini humo tangu wikiendi iliyopita na juzi Jumatatu alifanikiwa kusaini mkataba.
“Chirwa amejiunga na Ismailia baada ya kuafikiana makubaliano yao, hivyo ameachana rasmi na Yanga na sasa atakuwa mchezaji wa timu hiyo kuanzia sasa,” kilisema chanzo.
Meneja wa mchezaji huyo, Jonas Tiboroha, alipotafutwa hakuweza kupatikana kulitolea ufafanuzi suala hilo, lakini hivi karibuni alikiri kwamba Chirwa ameenda Misri kumalizana na moja ya timu ya ligi kuu nchini humo.
0 COMMENTS:
Post a Comment