June 20, 2018


Bao pekee katika mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay dhidi ya Saudi Arabia, limehitimisha safari ya michuano hiyo kwa Misri inayoongozwa na Mohamed Salah.
Uruguay imeshinda kwa bao 1-0 dhidi ya Saudi Arabia, shujaa akiwa ni Luis Suarez aliyewahi kuichezea Liverpool akiwa shujaa wa klabu hiyo, wakati huo.

Salah na Misri watapanda ndege kurejea nyumbani baada ya mechi yao ya mwisho ya kundi ikiwa ni ya kukamilisha.

Ushindi wa leo, umeipa Uruguay pointi sita na kujihakikishia kusonga hatua ya mtoano pamoja na wenyeji Urusi huku Misri na Saudi Arabia, wakitupwa nyumbani.

Uruguay: Muslera, Varela, Godin, Gimenez, Caceres, Sanchez (Nandez 82), Bentancur, Vecino (Torreira 59), Rodriguez (Laxalt 59), Suarez, Cavani
Goals: Suarez (23) 
Saudi Arabia: Alowais, Hawsawi, Albulayhi, Alburayk, Alfaraj, Bahbri (Kanno 75), Alshahrani, Otayf, Aljassam (Almoqahwi 44), Aldawsari, Almuwallad (Alsahlawi 78)











0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic