Linapofikia suala la kunyoa, tena mitindo ya kuvutia basi ujue kiungo Paul Pogba hawezi kulaza damu.
Maana ameamua kuungana na wenzake wa kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa na kumsafirisha kinyozi maarufu Ahmed Alsanawi kwa zaidi ya kilomita 1500 kwenda Urusi ili awanyoe.
Pogba amenyolewa vizuriii na kinyozi huyo tayari kwa mechi inayofuata baada ya kuwa shujaa kwa kufunga bao la pili katika mechi yao ya kwanza ya Kombe la Dunia ambayo walishinda kwa mabao 2-1 dhidi ya Australia.
Pamoja na Pogba, wengine ambao walipata huduma ya kinyozi huyo ni Benjamin Mendy, Ng’olo Kante ambaye alinyoa “unga” kama kawaida yake, Samuel Umtiti, Kylian Mbappe na Ousmane Dembele.
0 COMMENTS:
Post a Comment