June 28, 2018


Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amewaomba viongozi wa timu hiyo waongeze machungu zaidi kwa watani zao wa jadi Yanga.

Rage amefunguka na kueleza anafurahishwa namna ambavyo Simba wamekuwa wakilipiza kisasi kutokana na kusajili wachezaji ambao wamekuwa wamekuwa wakihusishwa kuhitajika Yanga.

Kupitia kituo cha Radio EFM, Rage ameeleza kuwa ni wakati mwafaka sasa wa Simba kuinyanyasa Yanga huku akielezea sakata la mchezaji Mbuyu Twite ambaye alikuwa akimyatia wakati akiwa Mwenyekiti wa Simba wakati huo na baadaye Yanga kuwazidi kete.

Rage amesema kitendo cha Yanga kuwachukulia Twite hakikumfurahisha na badala yake hawakuwa na namna kutokana na Yanga kuwa na nguvu za aliyekuwa mfadhili wa klabu hiyo, Mfanyabiashara, Yusuf Manji.

Kutokana na kukumbuka sakata la Twite, Rage amewaomba viongozi wa klabu hiyo wazidi kuwaongezea machungu watani zao Yanga ili wazidi kuumia kwa kusajili wachezaji ambao watakuwa tishio kuelekea msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa.

Kauli hiyo ya Rage imekuja mara baada ya Simba kumsajili Meddie Kagere aliyekuwa Gor Mahia FC pamoja na aliyewahi kuwa kipa wao wa zamani, ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga, Deo Munish 'Dida'

6 COMMENTS:

  1. Nakuunga mkono 100 per cent

    ReplyDelete
  2. Mchezo wa mpira ni uungwana na si visasi mkuu hsyupo sahihi

    ReplyDelete
  3. Kama ulivyofanya ndvy utakavyofanyiwa

    ReplyDelete
  4. Kwa Simba ni kisasi kwa Yanga halali siyo mkuu?

    Protas-Iringa

    ReplyDelete
  5. Rage wadanganye wasiokujua kwa sisi tunaokujua tunafahamu mchezo wote jinsi ulivyokuwa na hela uliyopiga,na sio Mbuyu Twite tu hata kwa Chuji na Okwi,ni bora ukae kimya badala ya kutuchefua na kutufanya tufunguke tangu michezo yako ulipokuwa FAT.Jiandae kupanda kizimbani kutoa ushahidi kwenye kesi ya akina Aveva maana mkondo ni mmoja

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic