June 28, 2018


Na George Mganga

Klabu ya Simba imewatambulisha rasmi wachezaji wake wapya iliowasajili wiki hii mbele ya waandishi wa habari katika makao makuu ya klabu hiyo yaliyoko Msimbazi, Kariakoo, Dar es Salaam.

Wachezaji hao ni pamoja na beki Pascal Wawa aliyewahi kuichezea Azam FC, Mlinda Mlango Deogratius Munish 'Dida' ambaye pia aliwahi kuichezea Yanga pamoja na Meddie Kagere kutoka Gor Mahia FC.


Kagere amekabidhiwa jezi namba jezi namba 14, Dida akipewa jezi namba 32 na Wawa akikabidhiwa namba 27.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, ameshindwa kuweka wazi juu ya mikataba waliyoingia na klabu lakini ikielezwa kuwa wamesaini miaka miwili kwa kila mmoja.

Baada ya utambulisho huo, Manara amefunguka na kueleza klabu imedhamiria kufanya usajili wa wachezaji hao ili kukipa nguvu kikosi cha Simba kwa ajili ya mashindano mengi ambao inakabiliwa nayo siku za usoni.

Kauli hiyo ya Manara imekuja kufuatia baadhi ya mashabiki na wadau wa soka kuhoji kwanini Simba inasajili wachezaji wengi na walioenda umri, lakini Manara amewakingia kifua kwa kueleza wana maana pana kufanya hivyo.

Manara ameeleza Simba itakuwa inakabiliwa na mashindano mengi hivyo inawapasa kuwa na kikosi kipana zaidi ukizingatia na ligi ijayo itakuwa na mechi nyingi kutokana na timu kuwa ishirini tofauti na mwanzo.


6 COMMENTS:

  1. Ligi kuwa na timu nyingi naana yake usajili wachezaji wenye mapafu, nadhani hapo Msemji amejikana nafsi

    ReplyDelete
  2. naangalia nyuso za kila mchezaji naona ni kama vile bad hawajapewa chao

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahaaaaa, umenichekesha sana ndugu, eti nyuso kama bado hawapewa chao

      Delete
  3. mara paaa....Simba yamtambulisha Papa Tishimbi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic