June 28, 2018


Na George Mganga

Wakili Patrick Gakumba, amefunguka na kueleza kuwa Yanga walimuita hotelini kwa ajili ya mazungumzo ya kumsajili mchezaji wake, Meddie Kagere, ambaye tayari ameshamalizana na klabu ya Simba.

Gakumba ameeleza kuwa ni kweli Yanga walifanya naye mazungumzo lakini mchezaji mwenyewe hakupenda kuichezea klabu hiyo na badala yake akaeleza mapenzi yake kuwa yapo Simba.

Wakala huyo amesema Yanga walimfuata akiwa Rwanda lakini mipango yao ikaweza kukwama kutokana na mchezaji mwenyewe kusema anahitaji kujiunga Simba.

"Kuna klabu nyingi ambazo zilikuwa zinamuhitaji Kagere ikwemo hao mnaotaniana nao 'Yanga' walinifuata Hotelini Rwanda lakini mchezaji mwenyewe akasema anaipenda Simba'' amesema.

Baada ya kuwakataa Yanga, Gakumba alifuata na viongozi wa simba kufanya naye mazungumzo kisha kuweza kuelewana naye na baada ya hapo wakafikia mwafaka wa kumsainisha mkataba wa miaka miwili akitokea Gor Mahia FC.


2 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic