Mshambuliaji nyota wa Gor Mahia ametua kimyakimya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kumalizana na mabingwa wa Tanzania Bara, Simba.
Kagere alikuwa akitakiwa Yanga ambao waliamini angetuliza mchungu ya moyo hasa katika ushambulizi lakini watani wao wa jadi wamewahi na kufanya naye mazungumzo tena kwa kumleta jijini Dar es Salaam.
Gor Mahia ndiyo mabingwa wa Kenya na mabingwa wa SportPesa Super Cup huku Kagere akiwa nimfungaji bora wa michuano hiyo.
Taarifa zinaeleza, Kagere alifanya mazungumzo na Kaimu Rais w Simba, Salim Abdallah jijini Dar es Salaam, leo.
"Kagere anakuja Simba, amezungumza na uongozi na mambo ni mazuri kabisa. Ataondoka kesho kurudi Kenya lakini kila kitu kimewekwa sawa kwa kuwa anamalizia mkataba wake na Gor Mahia.
"Hadi sasa yuko Dar es Salaam na ameonekana ana nia ya kuichezea Simba," kilieleza chanzo.
Kagera aliifunga Simba katika mechi ya fainali ya SportPesa Super Cup katika Uwanja wa Afraha mjini Nakuru, Kenya, hivi karibuni.
Wako wapi waliokuwa wakibeza eti hawezi kuja Simba kwakuwa mzee? Hivi uzee huku anakufunga magoli, kweli utamwacha mchezaji wa namna yake? Chukueni vikinda wachezesheni muone magoli yatakavyomiminwa kwenye kapu lenu. Karibu sana Kagere.
ReplyDeleteJe ndo mahitaji ya kocha? Bora kegere utasema kocha kamuona,,,Na huyo wawa je?
DeleteVikinda nimecheka lakini uko sahihi....
DeleteNasikia mkataba wake unaisha mwisho wa July. Anachokuja kufanya ni kuwasikilizia Simba wana dau gani lakini sio kusajili! Kwani Gor Mahia wanataka kumwongezea mkataba na mkwanja mrefuuuuu!
ReplyDeleteNaishauru yanga kuwa umefika wakati wa kwenda kutambika kutokana na kuelemewa na mikosi isiyomalizika. Hapa simba inaonesha kama inalipiza kisasi kutokana. na yale ambayo yanga ikiwafanyia katika zile siku zao za asali
ReplyDelete.
Ipo hatari kubwa inainyemelea yanga nao waijuee. Ligi haiko mbali sana kuanza, wachezaji waliomaliza mkataba wanakataa kuongeza na wale wapya wanaowataka kuwasili haraka wanapigwa pute na jee mambo yakiendelea hivi mpaka ligi kuu inaaza vipi itskuwa hali ya timu? Sasa mpira kote duniani ni pesa tu soo mambo kama yalivokuwa. hapo miaka hamsini iliuopita enzi za kina Sunday Manara na Mambosasa ambao wakicheza kwakugaiwa posho na mspenzi tu kwa timu zao wachezaji kama hao hakuna ila kabaki Ngasa tu. Wachwezaji wengi wamekuwa mamilionea duniani kote na mishahara ya mamilioni na hakuna cha bure
ReplyDeleteHapa inaonesha kama vile Simba inalipiza kisasi kwa yanga kutokana wakati ule ule wa maisha yao ya asali haraka yanga yanga ikiwachukuwa wachezaji wa simba kilaini na sasa imekuwa kils mchezaji yanga wanatamka kumtaka haraka wenye hela huwapiga pute kama walivokuwa wana fanya wao
ReplyDeleteThis is SIMBA
ReplyDelete