Hispania imefikisha pointi 4 baada ya ushindi wake wa kwanza wa bao 1-0 dhidi ya Iran leo na sasa inasubiri mechi yake ya mwisho dhidi ya Morocco.
Diego Costa ndiye aliyefunga bao pekee akigongeshewa mpira na beki wa Iran aliyekuwa akijaribu kuokoa.
Pointi 4 za Hispania zinawafanya kuwa na pointi sawa na Ureno na Iran inabaki kuwa na pointi zake tatu.
Maana yake, kuvuka katika kundi timu tatu za Ureno, Hispania na Iran zina nafasi wakati Morocco tayari imefungashiwa virago..
0 COMMENTS:
Post a Comment