Kocha wa Lipuli FC, Selemani Matola amesema wataendelea kutumia wachezaji wazawa ili kukiimarisha kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Matola amesema Lipuli FC hawana uwezo mkubwa wa kifedha ingawa angetamani kupata wachezaji wawili au watatu wa kimataifa.
"Kila kocha angetamani kuwa na wachezaji kutoka nje ya nchi, wachezaji bora zaidi ambao wangekuwa msaada. Lakini unajua hizi timu zetu, uwezo wa kifedha si mkubwa sana.
"Kama kocha nalitambua hilo, ndiyo maana tutaendelea kutumia wachezaji wazawa na tutafanya vizuri tu.
"Unajua wachezaji wazawa wako wengi sana wazuri ambao ni msaada mkubwa sana," alisema.
Lipuli FC ambayo ilipanda Ligi Kuu Bara tena msimu uliopita, ilimaliza katika nafasi ya saba na Matola amesema hawakutarajia kumaliza katika nafasi hiyo kwa kuwa lengo lao namba moja lilikuwa ni kubaki ligi kuu.
Kwani si tulisikia kuwa Matola kajiunga na Simba
ReplyDelete