June 28, 2018



Imeelezwa kuwa klabu ya Yanga iko kwenye nafasi nzuri ya kumsaini­sha kiungo mshambuliaji wa Azam FC, Paul Peter.

Habari za uhakika zinasema kwamba mchezaji huyo ameshafanya mazun­gumzo kinyemela na mchezaji huyo na hata viongozi wa klabu hiyo wameanza nao mazungumzo ambayo yapo kwenye hatua za awali.

Taarifa za uhakika zinasema kwamba Kamati ya Usajili ya Yanga chini ya Hus­sein Nyika na Kamati maalum ya uon­gozi chini ya Abbas Tarimba, wamepa­nia kuimarisha kikosi chake kwa kutwaa nyota mahiri kila idara ili kuwapa raha Wanayanga kuanzia msimu huu wa 2018/19.

“Usajili wetu ni wa kimyakimya,” alidokeza kigogo mmoja mwenye ush­awishi ndani ya kamati ya usajili huku akisisitiza kuwa wanamtaka Paul Peter kwa sifa mbalimbali.

“Bado ni kijana, ana uwezo, anajitam­bua, ana uwezo wa kufanya maamuzi. Ni nyota huwezi kufananisha na akina Ngoma (Donald).”

Yanga ina uhakika wa kupata saini ya Paul kutoka Azam kwani gharama za mkataba wake zinalipika. Mchezaji huyo aliingia mkataba wa miaka minne na Azam, Machi mwaka huu na kutambul­ishwa mbele ya wanahabari na ali­yekuwa Mtendaji Mkuu wa Azam, Abdul Mohammed.

Ngoma aliyetua Azam FC hivi karibuni hakuitumikia Yanga msimu uliopita, Paul yeye kwa upande wake alionesha umahiri mkubwa na Azam akifunga mabao mawili katika michezo miwili tofauti.

Miongoni mwa mechi hizo ni dhidi ya Singida United ambako aliingia katika dakika ya 84 na kuisawazishia Azam bao dakika za mwisho wa mchezo, hivyo ku­fanya matokeo kuwa sare ya 1-1 katika mchezo uliokuwa mgumu kwa Azam.

Dhidi ya Prisons alifunga bao la pili katika ushindi wa Azam wa mabao 2-0. Chipukizi huyo aliyeibuliwa mchangani katika mitaa ya Sinza na kocha anayelea vijana, Liston Katabazi ndiye ali­yeibuka kinara wa ufungaji bora katika mashindano ya Kombe la Mapinduzi msimu uliopita ambayo fainali zake zilichezwa Januari 13, mwaka huu.

Paul ndiye aliyeifikisha Azam robo fainali ya FA baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Shupavu ya Morogoro.

Mchezaji huyo ni miongoni mwa mas­taa wa Ngorongoro Heroes, walioku­wepo kwenye kikosi cha kufuzu Afrika dhidi ya Congo na Mali.

Katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mali uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Ngorongoro Heroes ililala kwa mabao 2-1 ambako bao la Tanzania lilifungwa na Paul Peter.

Na katika mchezo wa marudiano ulio­fanyika jijini Bamako, Mali Ngorongoro ilipoteza mchezo huo kwa mabao 4-1 ambako Paul Peter ndiye aliyekuwa mpishi wa bao la Tanzania kabla ya jopo la ufundi kumtangaza kuwa ndiye mchezaji bora wa mchezo huo.

Katika mashindano ya Uhai Cup yaliyofanyika Dodoma hivi karibuni, alikiwezesha kikosi cha Azam U20 kushika nafasi ya nne wakitolewa kwa matuta na vijana wa Simba. Paul Peter alifunga mabao matatu katika michezo mitano.

CHANZO: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic