June 16, 2018


Kali ya mwaka imetokea huko Nigeria kwa mashabiki wa timu ya taifa hilo kupigwa STOP na serikali kuhusiana na ombi lao la kutaka kwenda na kuku Uwanjani kuipa hamasa Super Eagles.

Kwa mujibu wa ripoti kutoka Nigeria, Waziri wa Utamaduni na Utalii nchini humo Andrei Ermak, amewazuia mashabiki hao ambao wlaipanga kusafiri na kuku hao kwa ajili ya kuisapoti timu yao.

Ermak amekataa ombi la mashabiki akieleza ni suala ambalo haliwezekani kuingia na kuku katika mashindano makubwa kama yale yanayofuatiliwa na dunia nzima.

Mashabiki hao walipelekea ombi hilo serikalini wakieleza kuwa huo ni utamaduni wao kufanya hivyo ili kuwapa hamasa wachezaji wao.

Ermak aligoma kuwasikiliza na kuwakatalia ombi lao huku aakiwaonya wasithubutu kufanya vile kutokana na ukubwa wa michuano hiyo namna ilivyo.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic