June 21, 2018





Kocha Juma Mwambusi amesema alikuwa na ndoto ya kuinoa Azam FC siku moja kwa kuwa ni moja ya timu bora barani Afrika.

Mwambusi amejiunga na Azam FC akiwa ni kocha msaidizi chini Hans van der Pluijm ambaye ndiye alimpendekeza.
Pluijm raia wa Uholanzi na Mwambusi waliwahi kufanya kazi pamoja katika kikosi cha Yanga na kufanikiwa kubeba ubingwa.

“Nilikuwa na ndiyo siku moja kucheza katika timu kama Azam FC, ni moja ya klabu bora barani Afrika,” alisema.

“Leo niko hapa, ninaamini nitafanya kazi kwa ushirikiano na wenzangu kuhakikisha tunapata mafanikio.”

Kabla ya kutua Yanga, Mwambusi alifanya vizuri akiwa na Mbeya City aliyoiwezesha kushika nafasi ya tatu ya Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza.

1 COMMENTS:

  1. Huyu atakuwa mbeba mipira na msemaji wa Pluijm. Ndivyo alivyokuwa Yanga��������

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic